Ijumaa 13 Juni 2025 - 14:39
Ghadir ni tafsiri halisi ya demokrasia ya kidini

Hawza/ Mwakilishi wa watu wa Gilan katika Baraza la Wataalamu wa Uongozi (Majlisi Khubragan Rahbari), Ayatollah Reza Ramadhani, amesisitiza juu ya umuhimu wa tukio la Ghadir na kusema kuwa "Ghadir ni tafsiri halisi ya demokrasia ya kidini".

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatollah Ramadhani, siku ya Alhamisi mchana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari na watu wa vyombo vya habari, alieleza kuwa; Mwenyezi Mungu ndiye aliyemtambulisha Imam Ali (as) kwa ajili ya dini, na lau Mtume Mtukufu (saw) hangelitangaza tukio hili, basi usingekamilika ujumbe wake wa Utume.

Amesema kuwa kuna mafundisho mawili makuu ndani ya tukio hili la muhimu katika jamii ya kibinadamu:

1. Watu bora zaidi ndio wanaopaswa kupewa majukumu muhimu.

2. Watu wanapaswa kuwa na nafasi ya kushiriki katika hatima yao.

Ustaadh Ramadhani ameifasiri Wilaya kuwa ni ulezi unaoambatana na mapenzi katika Uislamu, na akasema kuwa: Wilaya – kuanzia kwa Mtume (saw), Ma-Imamu Maasum (as), hadi Kiongozi wa Kidini (Waliyy Faqih) – inahusisha nyanja zote za jamii. Hivyo, Ghadir imekuja ili kuhakikisha kuwa watu wanashiriki katika kuamua mustakabali wao.

Akiashiria nafasi ya vyombo vya habari katika kufafanua dhana ya Kiislamu, amesema kuwa vyombo vya habari vya Magharibi kwa sasa vinafanya jitihada kubwa za kupotosha maana ya Wilaya na Ghadir kwa kutumia simulizi potofu. Amekazia kuwa njia ya kukabiliana na upotoshaji huo ni kuzalisha maudhui sahihi, kujibu shubuhati, na kufafanua kwa ufasaha mafundisho ya Kiislamu.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha